0% found this document useful (0 votes)
324 views4 pages

Mku - Sociolinguistics

Notes

Uploaded by

Mathias Kugaya
Copyright
© © All Rights Reserved
We take content rights seriously. If you suspect this is your content, claim it here.
Available Formats
Download as DOCX, PDF, TXT or read online on Scribd
0% found this document useful (0 votes)
324 views4 pages

Mku - Sociolinguistics

Notes

Uploaded by

Mathias Kugaya
Copyright
© © All Rights Reserved
We take content rights seriously. If you suspect this is your content, claim it here.
Available Formats
Download as DOCX, PDF, TXT or read online on Scribd
You are on page 1/ 4

1.

5 Lugha na Jamii

Isimujamii ni dhana ambayo imetokana na isimu na inaingtia lugha kama inavyotumiwa katika
jamii. Lugha si kifaa tu cha kuwasilisha habari bali ninamna muhimu ya kuanzisha na kudumisha
uhusiano miongoni mwa watu.

Kila tunapozungumza, wasikilizaji wetu hupata habari fulani kuhusu sehemu tunazotoka na sisi
ni watu wa aina gani. Hata mielekeo yetu na mawazo yetu vinaweza kutumiwa na wengine
kutuelewa zaidi.

Kiisimu, lugha sanifu haichukuliwi kuwa bora kuliko lahaja au lugha nyinginezo. Lugha zote
zina mifumo tata yenye kanuni za kipekee. Kule kusema kuwa lugha moja ni bora kuliko
nyingine ni jambo la kijamii, si la kiisimu.

Katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha na jamii, wataalamu wengi wamezungumzia
nadharia tete ya Sapir-Whorf (Edward Sapir na Benjamin Lee Whorf). Nadharia hii inaeleza
kuwa lugha asilia ya mtu hutawala jinsi anavyouelewa ulimwengu. Hii ina maana kwamba
tofauti za kiisimu huweza kuzusha utambuzi unaotofautiana. Ina maana kwamba hatuwezi
kuwaza bila lugha. Basi ikiwa mtu anaweza kudhibiti lugha wanayojifunza watu, atakuwa na
uwezo wa kudhibiti mawazo yao.

Kulingana na Sapir-Whorf (1956), binadamu huelewa mazingira kupitia kwa lugha


wanayoitumia. Wanatoa mfano wa Waeskimo ambao wana maneno mengi yanayoelezea hali
mbalimbali za theluji, huku Kiingereza kikiwa na neno moja tu snow.

Pia katika jamii ya Hopi, lugha yao inataja vitu kama mawingu na mawe kama vitu vilivyo hai.
Hali hii inawafanya waufikirie ulimwengu kwa njia tofauti na watu wengine.

Eneo analoishi mtu hujitokeza katika lugha yake hasa katika muundo wa msamiati. Kwa mfano,
mfumo wa aila katika jamii hujitokeza katika msamiati wa aila kama vile mtoto, binti, babu,
nyanya, shangazi, n.k.

Pia maadili ya jamii yanaweza kuwa na athari katika lugha ya jamii hiyo. Haya hutokea kupitia
kwa miiko. Miiko huhusika na tabia ambazo zimekatazwa katika jamii fulani. Maneno ambayo
ni mwiko katika lugha fulani hutuonyesha mfumo wa maadili na imani za jamii hiyo. Kwa hivyo
mwiko ni swala la kiisimu kama lilivyo la kijamii. Miiko husababisha maneno fulani kupotea
kutoka kwenye lugha na mengine kuzuka.

Kwa hivyo, isimujamii ni sehemu ya isimu inayoiangalia lugha kama sehemu ya kijamii na
utamaduni wa watu. Inachunguza nyanja za lugha na jamii, na ina uhusiano wa karibu na
taaluma nyingine kama anthropolojia, sosholojia, saikolojia na hata jiografia.

1.6 Isimujamii na Taaluma Nyingine


Si watafiti wa isimu na isimujamii pekee wanaohusika na uchunguzi wa lugha katika jamii.
Wataalamu kutoka kwa taaluma nyingine kama vile wanaanthropolojia, wanasaikolojia, n.k
huhusika pia.

1.61 Isimujamii na Saikolojia

Taaluma hizi mbili hushughulikia swala la mielekeo (attitudes) kuhusu aina Fulani za lugha.
Ingawa wanaisimujamii wanachunguza kwa kina swala la mielekeo kuhusu lugha, hili ni jambo
la kisaikolojia kwa kuwa lipo katika akili ya mtu.

Wanasaikolojia hutueleza jinsi mtoto anavyojifunza lugha kupitia kwa uwezo maalum
anaozaliwa nao (innate capacity), lakini pia lazima tufahamu jinsi tofauti za kimazungumzo (mf
kijinsia) zinavyokuzwa katika mchakato wa kuingiliana kijamii.

1.6.2 Isimujamii na Anthropolojia

Anthropolojia ni taaluma inayohusika na elimu ya binadamu, hususan elimu inayohusu habari za


asili na maendeleo yake ya awali. Inachukuliwa kuwa jinsi binadamu huyu alivyokua katika
kikundi, alikuwa anazungumza lugha fulani.

Wanaanthropolojia kadha wamefanya utafiti ambao una misingi ya kiisimujamii, kwa mfano,
kwa kuchunguza mfumo wa aila wa jamii. Tunajua kuwa mfumo wa aila hujitokeza katika
msamiati. Kwa mfano, utaona kuwa jamii nyingi za Kiafrika zina msamiati mpana unaoelezea
uhusiano wa kiaila kuliko lugha za Wazungu.

1.6.3 Isimujamii na Elimu

Wanaelimu wanatakiwa kutoa maamuzi kuhusu maswala yanayohusu lugha kama vile
ufundishaji wa lugha sanifu. Wanaisimujamii wamekuwa wakijaribu kushawishi wanaelimu
wabadili mielekeo yao kuhusu lugha Fulani zinazozungumzwa na watoto fulani shuleni kama
vile lugha zao za kwanza.

Wapangaji lugha huhitajika kuwa na ufahamu fulani wa kiisimu ili waweze kutoa uamuzi
unaofaa kuhusu aina ya lugha inayotakiwa kukuzwa na kuhimizwa katika miktadha fulani, daraja
na shule nk.

1.6.4 Isimujamii na Utamaduni

Wanaanthropolojia hushughulikia utamaduni ili kuweza kueleza tabia za watu za kiisimu;


wanaisimujamii huoanisha lugha na utamaduni kwa kuzingatia sarufi.

Uhusiano kati ya taaluma hizi mbili unatokana na ile haja ya kuyaelewa makundi mbalimbali ya
watu. Hivi ni kusema kwamba ni vigumu kwa wanaanthropolojia kuchunguza jamii za kale bila
kuzingatia lugha za watu hao; na pia ni vigumu kuchunguza lugha bila kuzingatia uamilifu wa
mazungumzo fulani katika jamii. Kwa hivyo lugha na utamaduni ni tabia za binadamu.

1.6.5 Isimu na Sosholojia (Elimujamii)

Wanaisimujamii hutalii miundo ya kijamii na namna miundo hiyo inavyoathiri lugha. Kuna
nguvu fulani za kijamii ambazo husababisha wanajamii kutaka kuongea au kutamka maneno kwa
njia fulani.

Uchaguzi wa kipashio Fulani cha kiisimu unatokana na jinsi jamii inavyochukulia kipashio
hicho. Lugha hutueleza mengi kuhusu mtu katika jamii.

1.7 Mitazamo ya Lugha

Wanazuoni mbalimbali wakiwemo Greenberg (1957), Hymes (1974), Dik (1978) n.k.
wanaiangalia lugha kwa mitazamo miwili: mtazamo wa kiisimu na ule wa kiisimujamii.

a. Katika mtazamo wa kwanza (wa kiisimu), lugha inaelezwa kuwa ni mfumo wa sauti
nasibu zinazotumiwa na watu wa jamii fulani wenye utamaduni unaofanana ili
kuwasiliana. Mtazamo huu unachukulia lugha kuwa kitu halisi ambacho kinaweza
kuainishwa katika vipande sauti vidogo vidogo ambavyo kwa pamoja huunda mfumo wa
lugha wa mawasiliano.

Chomsky (1957) aliunga mkono mtazamo huu. Katika kuifafanua lugha, alitofautisha hali ya
umilisi na utendaji.

Umilisi ni kile ambacho mzungumzaji anafahamu kuhusu lugha yake. Uwezo huu humwezesha
kuelewa na kutoa sentensi nyingi jinsi anavyotaka kuwasiliana.

Utendaji ni jinsi mzungumzaji anavyoitumia lugha. Kutokana na maelezo haya ni kama


Chomsky anatueleza kwamba tusiichunguze lugha katika matumizi yake, au hata jinsi
tunavyojifunza lugha, bila kwanza kufahamu lugha ni nini.

Hivyo basi ufafanuzi wa Chomsky wa lugha una upungufu kwani unaichukulia lugha kama kitu
kinachojitosheleza. Unaiondoa lugha kutoka kwenye jamii. Hapa ndipo isimujamii inapoingilia
ili ilete kipengele cha jamii katika lugha.

b. Mtazamo wa pili wa lugha ni wa kiisimujamii. Mtazamo huu unaangalia lugha kama


sehemu ya utamaduni wa jamii ulio na ruwaza ambazo hurithishwa na watu wenyewe
kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Mtazamo huu unaichukulia lugha kama mali ya jamii.
Wanaisimujamii wanakubaliana na fasiri hii ya pili ya lugha.

Zoezi
 Isimu jamii ni nini?

 Taja mikabala mitatu ya isimujamii na uonyeshe kwa kutoa mifano jinsi

inavyoingiliana na kutofautiana.

 Eleza uhusiano uliopo kati ya lugha na jamii.

 Isimujamii ni taaluma inayoingiliana na taaluma nyingi katika jamii.

Fafanua kauli hii.

You might also like